Kwa at-Tirmidhiy imekuja:

ويلٌ للأعقابِ من النَّارِ

“Ole visigino kutokana na Moto!”

220 – Imepokelewa pia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ويلٌ للأعقابِ وبطونِ الأقدامِ من النارِ

“Ole visigino na matumbo ya nyayo kutokana na Moto!”[1]

Hadiyth hii ambayo ameiashiria at-Tirmidhiy ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” na Ibn Khuzaymah i ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Abdullaah bin al-Haarith bin Juz’ az-Zubaydiy, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ilihali Ahmad ameipokea moja kwa moja kutoka kwake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/206)
  • Imechapishwa: 19/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy