Swali: Je, mwanamke anakuwa mwenye kulaaniwa anapoweka ´Abaa´ah juu ya mabega yake hali ya kujifananisha na wanaume?

Jibu: Kunakhofiwa juu yake, kwa sababu hii ni katika sifa za wanaume. Kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega yake ni katika mavazi staili za wanaume. Kwa hivyo haijuzu kwa mwanamke kujifananisha nao.

Swali: Je, kwa mfano mwanamke akivaa kepsi na akatembea kama wanaume anakuwa ni mwenye kulaaniwa?

Jibu: Ikiwa ni katika mavazi ya wanaume kanuni inayosema: ni mwenye kulaaniwa ikiwa ni katika mavazi ambayo ni maalum kwa wanaume.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23429/هل-تشبه-المراة-بالرجل-في-زيها-يوجب-اللعن
  • Imechapishwa: 19/01/2024