Swali: Kwa hivyo inafaa kumlaani mtu kwa dhati yake inapokuwa nyingi shari yake?

Jibu: Inafaa kumlaani inapokuwa nyingi shari yake. Ni kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyowalaani kikosi cha Quraysh kwa sababu ya shari yao. Hata hivyo kilichotangaa kutokana na kitendo na Sunnah zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kulaani kwa njia ya ujumla: Allaah amlaani mwizi, Allaah amlaani mzinzi, Allaah amlaani mla ribaa na Allaah amlaani mnywa pombe. Inatakiwa kuwa namna hii mtu alaani kwa njia ya sifa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23428/هل-يجوز-لعن-شخص-معين-لكثرة-شره
  • Imechapishwa: 19/01/2024