Swali: Je, swalah inaharibika iwapo maamuma atamtangulia imamu kwa nguzo moja au mbili?
Jibu: Iwapo maamuma atamtangulia imamu kwa makusudi, swalah yake inabatilika. Hata hivyo ikiwa ni kwa kutojua, anatakiwa kurudi na kumfuata imamu. Ikiwa maamuma alitangulia kwa makusudi, swalah yake inabatilika kwa mujibu udhahiri wa Hadiyth. Lakini [hapana vibaya] ikiwa ni kwa kutojua, kama vile kurukuu kabla ya imamu bila kujua, alipofundishwa akarudi kumfuata, au alileta Takbiyr kwa ajili ya kurukuu kabla ya imamu, alipofundishwa akarudi kumfuata.
Swali: Vipi ikiwa ni kwa kusahau?
Jibu: Anasamehewa ikiwa ni kwa kusahau pia.
Swali: Je, maneno ya wanazuoni kwamba mswaliji akimtangulia imamu kwa nguzo mbili ni sharti naye amtangulie kwa nguzo mbili?
Jibu: Sijui dalili inayothibitisha hilo. Katika swalah ya khofu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alirukuu na akasujudu. Alirukuu na wote kisha akasujudu na kundi la kwanza sijda mbili, kisha akasimama, kisha wakamfuata. Kwa msemo mwingine aliwatangulia kwa nguzo tatu: sujuud, sujuud na kikao baina ya Sujuud hizo mbili kutokana na udhuru.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24902/حكم-الماموم-اذا-سبق-الامام-بركن-او-ركنين
- Imechapishwa: 06/01/2025
Swali: Je, swalah inaharibika iwapo maamuma atamtangulia imamu kwa nguzo moja au mbili?
Jibu: Iwapo maamuma atamtangulia imamu kwa makusudi, swalah yake inabatilika. Hata hivyo ikiwa ni kwa kutojua, anatakiwa kurudi na kumfuata imamu. Ikiwa maamuma alitangulia kwa makusudi, swalah yake inabatilika kwa mujibu udhahiri wa Hadiyth. Lakini [hapana vibaya] ikiwa ni kwa kutojua, kama vile kurukuu kabla ya imamu bila kujua, alipofundishwa akarudi kumfuata, au alileta Takbiyr kwa ajili ya kurukuu kabla ya imamu, alipofundishwa akarudi kumfuata.
Swali: Vipi ikiwa ni kwa kusahau?
Jibu: Anasamehewa ikiwa ni kwa kusahau pia.
Swali: Je, maneno ya wanazuoni kwamba mswaliji akimtangulia imamu kwa nguzo mbili ni sharti naye amtangulie kwa nguzo mbili?
Jibu: Sijui dalili inayothibitisha hilo. Katika swalah ya khofu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alirukuu na akasujudu. Alirukuu na wote kisha akasujudu na kundi la kwanza sijda mbili, kisha akasimama, kisha wakamfuata. Kwa msemo mwingine aliwatangulia kwa nguzo tatu: sujuud, sujuud na kikao baina ya Sujuud hizo mbili kutokana na udhuru.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24902/حكم-الماموم-اذا-سبق-الامام-بركن-او-ركنين
Imechapishwa: 06/01/2025
https://firqatunnajia.com/maamuma-kumtangulia-imamu-kwa-nguzo-moja-au-mbili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)