Ni lini waswaliji wanatakiwa kusema ”Aamiyn”?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Na anaposema ”Aamiyn” nanyi semeni ”Aamiyn.'”

Ni lini waumini wanapaswa kusema ”Aamiyn”?

Jibu: Ni pale imamu anapoanza kusema ”Aamiyn”. Baada ya imamu kumaliza kusoma du´aa inayokusudiwa katika al-Faatihah, kwa sababu yote hiyo ni du´aa. Hapo ndipo wote wataitikia. Yeye ameomba du´aa kwa kusema:

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ

“Tuongoze njia iliyonyooka… ”

Imamu ameomba du´aa na huku waumini wamekaa kimya wakimsikiliza. Kisha baada ya hapo akasema:

وَلَا الضَّالِّينَ

“… wala waliopotea!”[1]

Watasema kwa pamoja ”Aamiyn”. Kwa sababu kuna upokezi mwingine unaosema:

”Anaposema:

وَلَا الضَّالِّينَ

“… wala waliopotea!”[2]

semeni ”Aamiyn.” Kwa sababu yeyote ambaye Aamiyn yake itaenda sambamba na Aamiyn ya Malaika basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”

Kwa hiyo lengo ni kuhakikisha Aamiyn yao iende sambamba na Aamiyn ya Malaika kwa namna ya kwamba wote waseme ”Aamiyn” kwa pamoja.

[1] 1:6-7

[2] 1:6-7

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24901/متى-يكون-تامين-المامومين
  • Imechapishwa: 06/01/2025