Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayekula kitunguu saumu au kitunguu maji basi atuepuke, au aepuke msikiti wetu, na aketi nyumbani kwake. Kwani hakika Malaika wanaudhika kwa yale yanayowaudhi wanadamu.”[1]

Hadiyth inafahamisha kuwa mwenye kula kitunguu saumu anapaswa kuwekwa mbali na msikiti na andolewe humo. Ikiwa sababu ya kumwondoa msikiti ni kwa sababu anawaudhi wengine, basi maudhi hayo yanaweza kulinganishwa na mengine yote yanayowaudhi majirani zake msikitini. Mfano wa hayo ni kama awe na mdomo mchafu, anawashambulia au kuwatukana watu msikitini, ananuka kwa sababu ya kazi yake au amebeba maradhi yanayonuka vibaya kama vile ukoma na mfano wake. Ikiwa mtu ana jambo ambalo linawaudhi watu na mtu huyo akawa msikitini na wakataka kumwondoa humo na kumweka mbali, basi wana ruhusa ya kufanya hivo muda wa kuwa sababu hiyo ipo. Wakati sababu inapoondoka basi inafaa kwake kurudi msikitini.

[1] al-Bukhaariy (7359).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Umar Yuusuf bin ´Abdil-Barr al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tamhiyd (6/422)
  • Imechapishwa: 02/10/2023