16 – ´Uyaynah bin ´Abdir-Rahmaan amesimulia kutoka kwa baba yake ambaye amesema:

”Mwanamke mmoja alikuja kwa Samurah bin Jundub na akamweleza kuwa mume wake hamuungi. Akamuuliza mwanamme yule ambaye akapinga jambo hilo. Baada ya hapo akamwandikia barua Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) akimuuliza juu ya kesi hiyo. Akajibu: ”Mpe mke na umfadhili kutoka katika wizara ya pesa. Mwache mwanamke huyo awe mzuri na dini yake. Mwanamke akidai kuwa anamuunga, basi waache waendelee kuishi pamoja, na kama mwanamke huyo anadai kuwa hamuungi, watenganishe.” Akafanya hivo na akawaleta nyumbani kwake. Asubuhi ilipoingia watu wakaingia na pia mwanamke yule akaingia. Akamwambia yule mwanamme ambaye alikuwa na alama ya zafarani: ”Umefanya nini?” Akajibu: ”Naapa kwa Allaah!  Nimefanya mpaka kukatetemeka ndani ya nguo zilizokuwa nyuma yake.” Mwanamke akaja amevaa shungi na akasimama karibu na miguu yake. Akamuuliza hivyohivyo. Mwanamke yule akakerwa na swali lile na kusema: ”Ndio, lakini anapokuwa karibu ndio huja shari yake.”Ndipo Samurah akasema: ”Mwache aondoke, ee Mtetemeshaji. Hii ni hukumu ya Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh).”[1]

[1] al-Bayhaqiy kwa cheni ya wapokezi nzuri. Nilikuwa nafikiri kuwa upokezi huu unafahamisha kuwa wanawake hapo katika zama za mwanzo walikuwa wakifunika nyuso zao, lakini ikanibainikia kuwa mambo ni kinyume. Kusema kwamba alikuwa amevaa shungi ni kwamba alikuwa amefunika kichwa chake, na si uso wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 02/10/2023