Kutoka ´Abdus-Sattar kwenda ´Abdus-Sittiyr

Swali: Mimi naitwa ´Abdus-Sattaar. Je, linafaa?

Jibu: Hakuna katika as-Saatir wala as-Sattaar lililothibiti, lililothibiti ni as-Sittiyr[1]. Bora ni ubadilishe kwenda katika ´Abdus-Sittiyr. Ni kweli kwamba miongoni mwa sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni kusitiri, lakini majina Yake hayathibitishwi isipokuwa tu kwa njia ya Qur-aan na Sunnah. Kwa ajili hiyo bora ni wewe kuitwa ´Abdus-Sittiyr, kwa sababu hilo ndilo jina lililopokelewa katika Sunnah.

[1] Ya´laa amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mtu akikoga sehemu ya wazi pasi na shuka ya chini. Hivyo akapanda juu ya mimbari, akamuhimidi Allaah na kumsifu. Kisha akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Allaah (´Azza wa Jall) ni Mwenye haya na Mwenye kusitiri (Sittiyr) na anapenda staha na kusitiri. Hivyo basi, atakapooga mmoja wenu ajisitiri.” (Abu Daawuud (4011). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abu Daawuud” (4011))

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=UoyQuRk1ik8
  • Imechapishwa: 02/10/2023