Swali 36: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni lini alifika Qubaa´?

Jibu: Jumatatu tarehe kumi na nane Rabiy´ al-Awwal. Hapo ndipo alipojenga msikiti wake uliokuwa umejengwa juu ya uchaji kuanzia siku ya kwanza ulipojengwa. Kwa mujibu wa maoni sahihi ndipo msikiti uliokusudiwa na Aayah (09:18). Ingawa msikiti wake aliyojenga Madiynah una haki zaidi ya kusifiwa namna hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 105
  • Imechapishwa: 02/10/2023