Kuwafanyia uchoyo wale ambao unalazimika kuwahudumia

Swali: Unasamaje juu ya yale yaliyotangulia “ni haramu kufanya uchoyo katika yale ambayo yanamlazimu mtu na ikiwa hayamlazimu basi inachikiza”. Ni ipi maana ya maneno haya?

Jibu: Haijuzu kwake kufanya uchoyo katika yanayomlazimu. Kitendo cha kuwafanyia uchoyo wale walioko chini yake, wakiwemo watoto na wake, na hawapati chenye kuwatosheleza ni jambo lisilojuzu. Ni lazima kwake kuwahudumia kile kinachowatosha. Lakini kuwahudumia watu wengine ni jambo linalopendeza. Hakuna kinachomlazimu isipokuwa zakaah, ambayo ni zakaah.

Swali: Nini maana ya kinachomlazimu?

Jibu: Akifanya uchoyo ilihali yuko na uwezo na watu wanahitaji ni jambo linachukiza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22287/حكم-من-يبخل-بما-يجب-عليه
  • Imechapishwa: 27/01/2023