Swali: Baadhi yetu huandika Aayah za makaa na sukari kwenye karatasi kisha wanaziweka ndani ya chombo kilicho na maji kisha wanakunywa. Ni ipi hukumu ya hili?

Jibu: Bora iwe kwa kitu kingine kisichokuwa makaa ima kwa zafarani au kitu kingine kisichodhuru. Hapana vibaya kufanya hivo. Hapana neno Aayah za Qur-aan zikiandikwa kwa zafarani kwenye karatasi au sahani kisha akanywa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22289/حكم-كتابة-ايات-ووضعها-في-ماء-للتداوي
  • Imechapishwa: 27/01/2023