Kuuza matunda kwenye mti kabla hayajakomaa

Swali: Vipi kuuza mtende kwa mtende mwingine?

Jibu: Hapana vibaya. Hapana vibaya kuuza mtende kwa mtende mwingine. Tunachokusudia ni kuuza matunda. Haifai kwa muuzaji kuuza matunda peke yake isipokuwa mpaka yakomae na kuiva. Hata hivyo akiuza mtende matunda ni yenye kuandamana nao. Katika hali hiyo matunda yanakuwa ya mnunuzi ikiwa wamekubaliana hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24440/هل-يجوز-بيع-النخل-بالنخل
  • Imechapishwa: 11/10/2024