Kuuza gari ambayo hujakuwa na nyaraka za umiliki

Swali: Vipi kwa ambaye ananunua gari na kuiuza kabla ya kuhamisha umiliki wake?

Jibu: Ni lazima aipokee kikamilifu na kuihamisha kutoka kwenye chumba chake cha maonyesho na kuipeleka sehemu nyingine. Kwa msemo mwingine inatakiwa kutimie umiliki wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuuza bidhaa pale kwenye kiwanda chake mpaka pale wafanyabiashara watapoifikisha sokoni. Asiuze kitu isipokuwa mpaka akimiliki kikamilifu na kwa mujibu wa njia iliyopangwa na serikali na maagizo ya serikali. Hatakiwi kwenda kinyume na maagizo ili kusitokee udanganyifu na khatari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24439/حكم-شراء-سيارة-ثم-بيعها-قبل-نقل-ملكيتها
  • Imechapishwa: 11/10/2024