Mdaiwa kulipa zaidi ya anachodaiwa

Swali: Vipi ikiwa mtu atachukua pishi 5 na akarudisha pishi 6 ila ya sharti?

Jibu: Anamaanisha kumfanyia wema, hapana ubaya. Hapana vibaya hata akimpa 100. Allaah amjaze kheri. Hata inapokuja katika dirhamu na dhahabu na fedha. Hapana vibaya akimuazima pauni 5 na akamrudishia pauni 6, akaazima kutoka kwake 100 SAR na akamrudishia 200 SAR. Hata hivyo lakini pasi na masharti wala kula njama yoyote.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24443/ما-حكم-رد-القرض-مع-زيادة-فوق-قيمته
  • Imechapishwa: 11/10/2024