Swali : Ni ipi maana ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayehiji na asifanye upuuzi wala kufanya ufuska, basi atarudi kutoka kwenye madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”[1]
Jibu: Mtu anapohiji na akaepuka yale ambayo Allaah amemharamishia katika kufanya upuuzi, ambao ni kule kujamii wanawake, na ufuska, ambao ni kwenda kinyume na utiifu, basi haachi yale ambayo Allaah amemfaradhishia na pia hafanyi yale ambayo Allaah amemharamishia. Ikiwa atakwenda kinyume, basi huo ndio ufuska. Hivyo mtu akihiji na asifanye ufuska wala upuuzi, hutoka katika Hajj hiyo akiwa safi na madhambi. Ni kama ambavyo mtoto anapotoka tumboni mwa mama yake hana dhambi yoyote. Basi vivyo hivyo mtu huyu akihiji kwa sharti hii, basi anakuwa ametakasika na madhambi yake.
[1] al-Bukhaariy (1521) na Muslim (1350).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/22)
- Imechapishwa: 08/05/2026
Swali : Ni ipi maana ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Yeyote atakayehiji na asifanye upuuzi wala kufanya ufuska, basi atarudi kutoka kwenye madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”[1]
Jibu: Mtu anapohiji na akaepuka yale ambayo Allaah amemharamishia katika kufanya upuuzi, ambao ni kule kujamii wanawake, na ufuska, ambao ni kwenda kinyume na utiifu, basi haachi yale ambayo Allaah amemfaradhishia na pia hafanyi yale ambayo Allaah amemharamishia. Ikiwa atakwenda kinyume, basi huo ndio ufuska. Hivyo mtu akihiji na asifanye ufuska wala upuuzi, hutoka katika Hajj hiyo akiwa safi na madhambi. Ni kama ambavyo mtoto anapotoka tumboni mwa mama yake hana dhambi yoyote. Basi vivyo hivyo mtu huyu akihiji kwa sharti hii, basi anakuwa ametakasika na madhambi yake.
[1] al-Bukhaariy (1521) na Muslim (1350).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/22)
Imechapishwa: 08/05/2026
https://firqatunnajia.com/hajj-ya-anayeepuka-ufuska-na-upuuzi/