Kutokata nywele wala kucha Dhul-Hijjah kwa atakayechinja

Yule aliyekusudia kuchinja katika ´Iydh-ul-Adhwhaa basi zinapoingia tu zile siku [kumi za mwanzo] za Dhul-Hijjah basi haifai kwake kukata chochote katika nywele na kucha zake isipokuwa mpaka baada ya kuchinja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zitapoingia zile siku kumi [za Dhul-Hijjah] na akataka mmoja wenu kuchinja, basi asichukue/asikate kutoka katika nywele wala kucha zake chochote mpaka achinje kwanza.”[1]

Akifanya chochote katika hayo basi amwombe msamaha Allaah na wala halazimiki kutoa fidia.

[1]Muslim.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mulakhaswsw-ul-Fiqh (01/151)
  • Imechapishwa: 12/07/2020