Swali: Muuliza huyu ni kutoka Uingereza anauliza kama inajuzu kwa mke wake kwenda kufunza Qur-aan Tukufu kwenye msikiti wa watu wa Bid´ah, Suufiyyah na Ahnaaf pamoja na kujua kuwa anahisi kuwa imani inaongezeka pindi anapofunza Qur-aan huko?

Jibu: Kufunza Qur-aan ni kulingania katika dini ya Allaah. Kile kitendo chake cha yeye kuwalingania watu wa Bid´ah na wale wenye upindaji, akawafunza Qur-aan na wakati huohuo akawalingania katika dini ya Allaah, akawafasiria Qur-aan na kuwawekea nayo wazi ni katika kulingania katika dini ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2136
  • Imechapishwa: 11/07/2020