Swali: ´Awwaam washirikina ambao wanaabudu makaburi na wanajikurubisha kwayo ni miongoni mwa wale waliofikiwa na Da´wah au watakuwa katika Ahl-ul-Fatrah?

Jibu: Ametakasika Allaah. Ni katika Ahl-ul-Fatrah ilihali wamehifadhi na wanasikiliza Qur-aan? Wamefikiwa na hoja. Ahl-ul-Fatrah ni wale ambao hawakusikia na wala hawakufikiwa na kitu. Ni watu ambao ulimwengu umekatika na wao. Hili halipatikani leo. Kuna yeyote ambaye ulimwengu umemkatikia? Vyombo vya khabari leo vimefika mashariki na magharibi. Hakuna yeyote ambaye [ulimwengu] haumfikii.

Lau tutakadiria kuna yeyote ambaye vyombo vya kisasa havimfikii na hafikiwi na kitu, atakuwa katika Ahl-ul-Fatrah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 11/07/2020