Kutoka mwanafunzi kuishilia kunyoa ndevu na kuvuta sigara

Swali: Mtoto wangu ana umri wa miaka 25. Alikuwa ni mwanafunzi mwenye kuanza. Baadaye akaacha elimu na kuanza kufanya kazi. Kisha akanyoa ndevu na kuvuta sigara. Matokeo yake nikamfukuza nyumbani na kumsusa. Je, kitendo changu hichi ni sahihi?

Jibu: Ndio. Akiwa anaweza kujisimamia na kuishi mwenyewe na hasikilizi nasaha, mfukuze. Lakini akiwa hawezi kuishi mwenyewe na pengine ndio akapotea na kuharibika zaidi, basi wewe mbakize nyumbani kwako, mchunge na mnasihi na usivunjike moyo wa kuongoka kwa idhini ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 15/06/2015