Swali: Kama kuna maoni mbili juu ya jambo fulani na yote mawili yakawa na nguvu kwa wanachuoni…

Jibu: Ni jambo lisilowezekana maoni yote mawili yenye kutofautiana yakawa na nguvu kwa wanachuoni. Hili ni jambo lisilowezekana. Katika hali hii hakuna maoni yanayotakiwa kutendewa kazi isipokuwa yale yaliyosimama juu ya dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah kuhusiana na maoni haya mawili au hata yakiwa mengi.

Swali: Je, nimkataze na kumlazimisha yale niliyofuata mimi katika jambo hili?

Jibu: Usisemi yale uliyofuata wewe. Unachotakiwa kusema ni kumlazimisha kwa yale yaliyosimama juu ya dalili. Ikiwa dalili zenye nguvu ziko na yeye wewe ndiye unatakiwa kumfuata. Ikiwa dalili zenye nguvu ziko na wewe yeye ndiye anatakiwa kukufuata. Kinachofuatwa ni dalili na sio maoni ya fulani na fulani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf-14-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2015