Msimamo juu ya maovu katika miji isiyohukumu kwa Shari´ah

Swali: Ni lipi la wajibu kwa mwenye kuona baadhi ya madhambi makubwa yanafanywa katika mji usiohukumu kwa Shari´ah ya Kiislamu?

Jibu: Yakataze kiasi cha uwezo wako:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

“Yule miongoni mwenu atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake na hiyo ni imani dhaifu mno.”[1]

Ayakataza kiasi cha uwezo wake.

[1] Muslim (49).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 15/06/2015