Swali: Kuswali swalah ya usiku kwa mkusanyiko ni jambo limewekwa katika Shari´ah? Ni ipi hukumu ya kudumu juu ya jambo hilo?

Jibu: Hakuna vibaya kuswali swalah ya usiku kwa mkusanyiko. Hata hivyo si jambo limewekwa katika Shari´ah kudumu katika jambo hilo; isipokuwa katika Tarawiyh ndani ya Ramadhaan. Kuhusu miezi mingine ndani ya mwaka ikitokea baadhi ya nyakati, pasi na kuchukulia hilo kama desturi, hapana vibaya. Mfano wake ni mtu kumswalisha mke wake, akawatembelea watu ambapo wakaswali mkusanyiko. Katika hali hizo hapana vibaya. Ama kufanya jambo hilo kuwa ni ada na Sunnah ni kitu hakina msingi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9955/حكم-صلاة-الليل-جماعة-والمداومة-على-ذلك
  • Imechapishwa: 06/04/2023