al-Ikhlaasw katika Rak´ah zote za Tarawiyh

Swali: Kuna baadhi ya vijiji vidogo katika swalah ya Tarawiyh mwezi wa Ramadhaan imamu anasoma Aayah moja au Aayah mbili katika kila Rak´ah na wengine katika Rak´ah zote anasoma Qul huwa Allaahu Ahad. Je, swalah inasihi kwa hali hiyo?

Jibu: Swalah ni sahihi. Lakini bora ni yeye kuwasomea kuanzia mwanzoni mwa Qur-aan kile kitachomkuwia chepesi. Akiweza kuwasomea Qur-aan yote ndio bora na kamilifu zaidi. Lakini kuhusu kusihi inasihi akiwasomea baadhi ya Aayah au sehemu ya Suurah. Yote hayo hayana neno:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ

“Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan.”[2]

Hakuna kikomo maalum cha kisomo katika swalah ya Tarawiyh. Bali asome kitachomsahilikia baada ya al-Faatihah.

Mwendesha kipindi: Vipi kitendo cha kusoma Suurah al-Ikhlaasw katika kila Rak´ah?

Ibn Baaz: Hapana neno akiwa hana zaidi ya hiyo. Lakini akiwa na kingine bora ni yeye kusoma pia kutoka katika Suurah zingine na Qul huwa Allaahu Ahad aisome katika Witr peke yake katika ile Rak´ah ya mwisho. Hivi ndio bora.

[1] 64:16

[2] 73:20

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9890/حكم-من-يقرا-في-التراويح-باية-او-ايتين-في-الركعة
  • Imechapishwa: 06/04/2023