Swali: Wako ambao wanachukulia wepesi kwa njia ya kwamba wanalala wakati wa swalah ya Fajr na swalah ya ´Aswr. Hawazikanushi. Wanaziswali pale wanapaomka.

Jibu: Wakikusudia wanakufuru kwa jambo hilo. Ama usingizi ukiwashinda basi wanapaswa kuharakisha kuswali wanapoamka. Lakini wakifanya kwa makusudi kwa njia ya kwamba akaweka alamu ya kumuamsha pale utapofika wakati wa kwenda kazini na vivyo hivyo ´Aswr akaiacha kwa makusudi, huyu anakufuru kwa kufanya hivo.

Swali: Hata kama hafanyi hivo kila siku?

Jibu: Haijalishi kitu. Anakufuru kwa ile mara ya kwanza tu. Kila atavyozidi kuiacha ndivo unavyozidi ukafiri wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22509/ما-حكم-التهاون-بصلاتي-الفجر-والعصر
  • Imechapishwa: 30/06/2023