Kafiri kwa kuacha swalah moja tu makusudi

Swali: Vipi mtu endapo atachukulia wepesi kuacha swalah moja peke yake?

Jibu: Kwa mujibu wa maoni sahihi anakufuru. Kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni ni kwamba anakufuru ingawa kwa kuacha swalah moja tu. Hapa ni pale ambapo ataiacha kwa makusudi mpaka ukatoka wakati wake. Ni lazima kwake kutubu na kurejea kwa Allaah. Akitubu basi Allaah atamkubalia tawbah yake.

Swali: Vipi kuacha swalah ya ´Aswr?

Jibu: Ni mamoja Fajr, Dhuhr na nyenginezo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22506/حكم-من-ترك-صلاة-واحدة-تهاونا-وكسلا
  • Imechapishwa: 30/06/2023