“Hawakufuru kwa sababu wanatamka shahaadah”

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa asiyeswali au anaswali baadhi ya nyakati tu au anaacha kuswali baadhi ya nyakati tu kwamba sio kafiri hata hivyo ni mtenda dhambi.

Jibu: Haya ni maoni ya baadhi ya wanazuoni. Maoni ya sawa ni kwamba anakufuru kwa jambo hilo kutokana na Hadiyth zilizotajwa. Tunamuomba Allaah usalama.

Swali: Vipi kwa wanaosema kuwa hakufuru kwa sababu wanatamka shahaadah?

Jibu: Waraddiwa kwa kuambiwa kwamba anayetamka shahaadah ni lazima aitekelezee haki yake. Miongoni mwa haki zake ni kuchunga vipindi vitano vya swalah ndani ya nyakati zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22510/حكم-من-لا-يصلي-ومن-يتركها-احيانا
  • Imechapishwa: 30/06/2023