Swali: Je, katika Hadiyth ya Abu Rifaa´ah kunachukuliwa hukumu kwamba haina neno kwa imamu kukata Khutbah akihitaji kufanya hivo?

Jibu: Ndio, aikate kutokana na haja iliyozuka na baadaye aikamilishe. Mfano wa haja hizo ni kumzindua mtu juu ya khatari inayomkabili, kukemea maovu na mengineyo. Ni kama ambayo siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoa Khutbah ambapo akaingia mtu na kuketi chini akamwambia:

”Simama na uswali Rak´ah mbili.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22339/حكم-قطع-الامام-خطبة-الجمعة-لحاجة
  • Imechapishwa: 10/02/2023