37. Dalili kuthibitisha kuwa shauku, woga na unyenyekeaji ni ´ibaadah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya shauku, woga na unyenyekeaji ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.”[1]

MAELEZO

Shauku maana yake ni kuomba na unyenyekevu pamoja mapenzi ya kufikia kitu kinachopendwa. Ikiwa anaomba na wakati huohuo akawa na nguvu ya kukifikia kile anachokitaka, basi hiyo ndio shauku.

Woga ni kujitenga mbali kwa njia ya kuyakimbia yale yanayochukiza. Hivo ndivo amesema Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) pia[2]. Ni khofu yenye kuambatana na kitendo. al-Aswfahaaniy amesema:

“Woga ni khofu pamoja na kujilinda.”[3]

Unyenyekevu ni kule kujidhalilisha. Ina maana vilevile ya kunyenyekea (الخضوع). Isipokuwa kunyenyekea kwa maana hii mara nyingi inakuwa katika mwili na unyenyekevu aina ya kwanza unakuwa moyoni au sauti. Amesema (Ta´ala):

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ

“Hakika wamefaulu waumini; ambao katika swalah zao ni wenye kunyenyekea.”[4]

وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ لِلرَّحْمَـٰنِ فَلَا تَسْمَعُ إِلَّا هَمْسًا

“Sauti zitafifia kwa Mwingi wa rehema, basi hutosikia isipokuwa mchakato wa nyayo.”[5]

خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ

”Macho yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika.”[6]

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ

“Je, haujafika wakati kwa walioamini zinyenyekee nyoyo zao kwa ukumbusho wa Allaah na yale yaliyoteremka ya haki.”[7]

Maeneno Yake (Ta´ala):

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.”

Matumaini ikiwa na maana ya wakitaraji yale yalioko Kwake. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

”Tofauti kati ya matumaini na matarajio ni kwamba kutaraji ni kule kutamani na kutamani ni kule kutaka na ndio kinachozalishwa na matarajio. Mtu anapoataraji kitu basi hukitaka. Matumaini ukiyalinganisha na matarajio ni kama kukimbia kutokana na khofu.”[8]

Aayah hii imejulisha aina zote tatu za ´ibaadah, kama itakavyobainika kwa kutaja. Kuwa na shauku, woga na kunyenyekea anatakiwa kufanyiwa mambo hayo Allaah pekee. Kwa msemo mwingine haifai kwa mtu akamuonea shauku mwingine asiyekuwa Allaah na wala asimuogope isipokuwa Yeye. Makusudio ya shauku na woga ni kwa aina ya ´ibaadah. Shauku na woga havisimami isipokuwa kwenye shina la subira. Woga wa mtu unampelekea kufanya subira na shauku yake inamvuta kushukuru. ´Ibaadah ya shauku na woga zinapungua kwa mja kwa kiasi cha madhambi yake na zinaongezeka kwa kupanda imani yake. Matokeo yake anawafikishwa – kwa idhini ya Allaah – kwa kiasi cha ´ibaadah hizo. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

”Akimtakia mja Wake kheri basi anamuwafikisha kutumia wakati na uwezo wake na kujipinda katika kumuonea shauku na kumuogopa. Mambo hayo mawili ndio nyenzo za kuwafikishwa. Kwa kadiri ya ile shauku na woga uliosimama moyoni ndio kunapatikana maafikisho.”[9]

[1] 21:90

[2] Madaarij-us-Saalikiyn (01/508).

[3] Tazama ”Mufradaat fiy Ghariyb-il-Qur-aan” (366).

[4] 23:01-02

[5] 20:108

[6] 68:43

[7] 57:16

[8] Madaarij-us-Saalikiyn (02/55).

[9] Shafaa´-ul-´Aliyl, uk. 107.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 11/02/2023