Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya tisho ni Kauli Yake (Ta´ala):

فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي

“Hivyo basi msiwaogope bali niogopeni.” [1]

MAELEZO

Tisho maana yake ni khofu. Lakini tisho ni maalum zaidi kuliko khofu. Kwa sababu tisho imeambatana na kuwa na utambuzi juu ya Allaah. Amesema (Subhaanahu wa Ta´aal):

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si vyenginevyo wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.”[2]

Tisho ni khofu iliyoambatana na kuwa na kumjua Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwa Allaah kwamba mimi ndiye namukhofu na kumcha Allaah zaidi kuliko nyinyi.”[3]

Shaykh ´Abdur-Rahmaan as-Sa´diy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Khofu, tisho, unyenyekevu na woga maana zake zinakaribiana. Khofu inamzuia mtu kutokana na yale aliyoharamisha Allaah na tisho inashirikiana nayo katika jambo hilo. Isipokuwa tisho imeambatana na kumtambua Allaah. Kuhusu unyenyekevu na woga yanatokamana na kumukhofu na kumuogopa Allaah. Matokeo yake mja anamnyenyekea Allaah na kujishusha kwa Mola wake hali ya kurejea Kwake kwa moyo wake na jambo hilo linazalisha woga. Ama kuhusu unyenyekevu ni ule uhudhuriaji wa moyo wakati wa kumtii Allaah na kutulia kwa nje na kwa ndani kwake, kitu ambacho ndio unyenyekevu maalum. Kuhusu unyenyekevu wa kudumu ambao ndio sifa ya wale waumini maalum unazalika kwa mja kumtambua Mola wake na kutambua kwake kuwa anamchunga. Kwa hivyo jambo hilo linautawala moyo kama yanavyotawala mapenzi.”[4]

Maneno Yake (Ta´ala):

فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي

“Hivyo basi msiwaogope bali niogopeni.”

Bi manaa msiwaogope watu woga wa ´ibaadah.

Kinachokusudiwa katika Aayah ni kwamba mtu akimuogopa mwingine asiyekuwa Allaah  ile khofu aina ya ´ibaadah inayoutuliza moyo wake ambayo inamfanya kutii na kujiepusha na maasi, basi khofu hii ni miongoni mwa aina ya shirki. Kwa sababu Allaah ameifanya ni miongoni mwa mambo mambo yanayopelekea imani. Mwenye kumtekelezea aina hii asiyekuwa Allaah sio muumini.

[1] 02:150

[2] 35:28

[3] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1108).

[4] Tazama ”Taysiyr-ul-Kariym-ir-Rahmaan” (02/362).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 11/02/2023