Swali: Je, inapaswa kufuata mpangilio katika Tayammum?

Jibu: Huu ndio msingi khaswa inapokuja katika wudhuu´. Lakini ni bora mtu afanye kama alivyofanya katika wudhuu´, kwa sababu yeye alifanya Tayammum kuwa ni kitu kimoja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya ni kitu kimoja. Muumini anatakiwa kufanya kama alivyoamrishwa na Allaah. Lakini ikiwa mtu atazingatia msingi huo katika josho na asipangilie, udhahiri ni kwamba inatosha katika josho la janaba. Hata hivyo atakuwa ameenda kinyume na kilicho bora zaidi. Inavyopaswa katika Tayammum ni yeye kufanya kama ilivyoelezwa katika Aayah:

فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

”… basi fanyeni Tayammum kwa ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Vilevile kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Ammaar. Ni mamoja iwe kwa ajili ya janaba au kwa ajili ya hadathi ndogo, kwa sababu amepunguza ugumu na kurahisisha na kufanya kuwa ni kitu kimoja.

[1] 04:43

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24765/حكم-الترتيب-في-التيمم
  • Imechapishwa: 23/12/2024