27. Kama mtu anampenda Abu Hurayrah na Ahmad bin Hanbal

139 – Ukimuona mtu anahifadhi swalah za faradhi na mkusanyiko pamoja na mtawala na wengineo, basi tambua kuwa ni mtu wa Sunnah – Allaah (Ta´ala) akitaka. Na ukimuona mtu anapuuza swalah za faradhi na mkusanyiko, hata kama itakuwa pamoja na mtawala, basi tambua kuwa ni mtu wa matamanio.

140 – Mambo ya halali ni yale uliyoyashuhudia na ukaapa kwayo ya kwamba ni halali na vivyo hivyo mambo ya haramu. Yale yenye kutia shaka kifuani mwako ni yenye utata.

141 – Msitiriwa ni yule ambaye sitara yake imethibitishwa, na mfedheheshwa ni yule ambaye fedheha yake imethibitishwa.

142 – Ukimsikia mtu anasema “Fulani ni Mushabbih, fulani anatamka kwa Tashbiyh”, basi mtuhumu na ujue kuwa huyo ni Jahmiy.

Ukimsikia mtu anasema “Fulani ni Naaswibiy”, basi tambua kuwa huyo ni Raafidhwiy.

Ukimsikia mtu anasema “Zungumza kwa Tawhiyd! Nifafanulie Tawhiyd”, basi tambua kuwa huyo ni Khaarijiy, Mu´taziliy.

Akisem”a “Fulani ni Mujbir au anazungumza kwa kutenzwa nguvu au uadilifu”, basi tambua kuwa huyo ni Qadariy, kwa sababu majina yote haya yamezushwa na watu wa matamanio.

143 – ´Abdullaah bin al-Mubaarak amesema:

“Usichukue chochote kinachohusiana na ´Aqiydah ya Raafidhwah kutoka Kuufah. Usichukue chochote kinachohusiana na upanga kutoka Shaam. Usichukue chochote kinachohusiana na makadirio kutoka Basrah. Usichukue chochote kinachohusiana na ´Aqiydah ya Murji-ah´ kutoka Khuraasaan. Usichukue chochote kinachohusiana na biashara ya dhahabu na fedha kutoka Makkah. Usichukue chochote kinachohusiana na nyimbo kutoka Madiynah. Usichukue chochote kutoka kwao kuhusiana na mambo hayo.

144 – Ukimuona mtu anampenda Abu Hurayrah, Anas bin Maalik, Usayd bin Hudhwayr, basi tambua kuwa ni mtu wa Sunnah – Allaah akitaka.

Ukimuona mtu anampenda Ayyuub, Ibn ´Awn, Yuunus bin ´Ubayd, ´Abdullaah bin Idriys al-Awdiy, ash-Sha´biy, Maalik bin Mighwal, Yaziyd bin Zuray´, Mu´aadh bin Mu´aadh, Wahb bin Jariyr, Hammaad bin Salamah, Hammaad bin Zayd, Maalik bin Anas, al-Awzaa´iy na Zaaidah bin Qudaamah, basi tambua ya kuwa ni mtu wa Sunnah.

Ukimuona mtu anampenda Ahmad bin Hanbal, al-Hajjaaj bin Minhaal na Ahmad bin Naswr, akawataja kwa uzuri na akafuata maoni yao, basi tambua kuwa ni mtu wa Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 117-121
  • Imechapishwa: 23/12/2024