134 – Ukimuona mtu anamtukana yoyote katika Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi tambua ya kwamba ni mtu mwenye maoni maovu na ni mtu mwenye kufuata matamanio yake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wanapotajwa Maswahabah zangu, basi nyamazeni.”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijua watayoteleza baada ya kufa kwake, lakini hakusema juu yao isipokuwa kheri. Amesema:
“Waacheni Maswahabah zangu na msiseme juu yao isipokuwa kheri tu.”[1]
Usizungumze kitu juu ya kuteleza kwao, vita vyao wala yale ambayo elimu yake imejificha kwako. Usimsikize yeyote anayeyazungumzia, hakika moyo wako hautasalimika endapo utasikiza kitu.
135 – Ukimsikia mtu anayatukana au kuyarudisha masimulizi au anatamani kitu kingine mbali na masimulizi, basi utuhumu Uislamu wake na usishuku kuwa ni mtu mwenye kufuata matamanio na mzushi.
136 – Tambua kuwa makandamizo ya mtawala hayapunguzi zile faradhi alizoweka Allaah (´Azza wa Jall) kupitia kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Udhalimu wake ni kwa nafsi yake. Matendo yako na utiifu wako wa Sunnah ni mtimilifu – Allaah (Ta´ala) akitaka. Kwa maana ya kwamba swalah ya mkusanyiko, swalah ya ijuma na jihaad inatakiwa kufanywa pamoja nao. Shirikiana naye katika aina zote za utiifu – uko pamoja na nia yako.
137 – Ukimuona mtu anaomba du´aa dhidi ya mtawala, basi tambua kuwa ni mtu anayefuata matamanio. Ukimuona mtu anamuombea mtawala du´aa ya kutengemaa, basi tambua kuwa ni mtu wa Sunnah – Allaah akitaka. Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Lau mimi ningelikuwa na du´aa yenye kuitikiwa, basi nisingeiweka kwengine isipokuwa kwa mtawala.”
Ahmad bin Kaamiyl amesema:al-Husayn bin Muhammad at-Twabariy amehadithia, kutoka kwa as-Swaa-igh, ambaye amesema: Nimemsikia Fudhwayl akisema:
“Lau mimi ningelikuwa na du´aa yenye kuitikiwa, basi nisingeiweka kwengine isipokuwa kwa mtawala.” Kukasemwa: “Ee Abu ´Aliy, tufafanulie hili!” Akasema: “Nikijiombea mwenyewe, itakuwa ni kwangu pekee. Nikimuombea mtawala na akanyooka, basi watanyooka vilevile waja na miji kupitia kutengemaa kwake.”
Tumeamrishwa kuwaombea kutengemaa na hatukuamrishwa kuomba dhidi yao, hata kama watadhulumu na kukandamiza. Hili ni kwa sababu ukandamizaji na dhulumu zao ni juu yao wenyewe, ilihali kutengemaa kwao ni kwa manufaa yao wao na waislamu.
138 – Usimtaje yeyote katika mama wa waumini isipokuwa kwa kheri tu.
[1] al-Bazzaar katika “Kashf-ul-Astaar” (03/290).
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 115-117
- Imechapishwa: 23/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 115-117
Imechapishwa: 23/12/2024
https://firqatunnajia.com/26-ukimuona-mtu-anayemuombea-duaa-nzuri-au-mbaya-mtawala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)