127 – Inatakiwa kuwasalimia waja wa Allaah wote.

128 – Ambaye anaacha swalah ya ijumaa na ya mkusanyiko msikitini bila ya udhuru wowote, ni mzushi. Miongoni mwa nyudhuru kunaingia pia maradhi yenye kumzuia mtu kutoweza kwenda msikitini au kumuogopa mtawala mwenye kudhulumu. Yasiyokuwa haya hayazingatiwi kuwa ni udhuru wowote.

129 – Yule mwenye kuswali nyuma ya imamu na asimfuate, swalah yake si sahihi.

130 – Kuamrisha mema na kukataza maovu kunakuwa kwa mkono, mdomo na moyo, bila ya upanga.

131 – Muislamu aliyesitiriwa ni yule asiyedhihirisha kitu kinachotia mashaka.

132 – Elimu yoyote ya ghaibu ambayo mja anatamka kwayo na si yenye kupatikana ndani ya Qur-aan wala Sunnah, ni Bid´ah na upotevu. Haimpasi yeyote kuitendea kazi wala kulingania kwayo.

133 – Mwanamke yeyote mwenye kujioza mwenyewe kwa mwanaume si halali kwake, isipokuwa kwa kuwepo walii, mashahidi wawili waadilifu pamoja na mahari. Katika hali nyinginezo wanatakiwa kuadhibiwa endapo watafanya kitu.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 113-115
  • Imechapishwa: 23/12/2024