121 – Inatakiwa kunyamazia vita vilivyotokea kati ya ´Aliy na Mu´aawiyah, ´Aaishah, Twahlah, az-Zubayr pamoja na wale waliokuwa pamoja nao. Usigombane kwa ajili yao. Liacheni jambo lao kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala), kwani hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jihadharini na kuwataja vibaya Maswahabah wangu, mashemeji zangu na wakwe zangu.”[1]
Vilevile amesema:
“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amewatazama watu wa Badr akasema: “Fanyeni mtakacho. Nimekusameheni.””[2]
122 – Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba si halali kuichukua mali ya muislamu, isipokuwa kile anachokitoa kwa ridhaa yake mwenyewe. Ikiwa mtu ana mali aliyoichuma kwa njia ilio ya haramu, jukumu liko kwake mwenyewe. Si halali kwa yeyote kuchukua kitu kutoka kwake isipokuwa kwa idhini yake. Huenda mtu huyu akatubia na akataka kuirudisha kwa wenyewe, hivyo utakuwa umechukua kitu kilicho cha haramu.
123 – Mapato na machumo yanachukuliwa kutoka katika yale ambayo usalama wake umebainishwa. Ni halali kabisa isipokuwa tu yale ambayo ufisadi wake umedhihiri. Endapo ni fisadi, atachukua yale yenye kutimiza haja yake. Asisemi kwamba anaacha kuchuma na badala yake akategemea kupewa na watu wengine. Haya hayakufanywa na Maswahabah wala wanazuoni mpaka hii leo. ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Chumo lililo na sehemu ya uchafu ni bora kuliko kuwahitajia watu.”[3]
124 – Swalah tano zinajuzu nyuma ya yule unayeswali nyuma yake, isipokuwa ikiwa kama atakuwa mtu Jahmiy, hakika huyo ni mkanushaji. Endapo utaswali nyuma yake basi irudie swalah yako. Ikiwa imamu siku ya ijumaa ni mtu Jahmiy na ndiye mtawala, swali nyuma yake na irudie swalah yako. Lau imamu atakuwa ni mtawala, au mtu mwengine, na akawa ni mwenye kufuata Sunnah, swali nyuma yake na wala usiirudie swalah yako.
125 – Inatakiwa kuamini kwamba Abu Bakr na ´Umar pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) chumbani kwa ´Aaishah. Walizikwa pamoja naye. Ukiliendea kaburi, basi unatakiwa kuwasalimia baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
126 – Ni wajibu kuamrisha mema na kukataza maovu, isipokuwa ambaye unachelea upanga au bakora yake.
[1] Si Swahiyh kwa mujibu wa ar-Raajihiy katika “Sharh Kitaab-is-Sunnah lil-Barbahaariy” (13/2).
[2] al-Bukhaariy (3006) na Muslim (2494).
[3] Iswlaah-ul-Maal (321) ya Ibn Abiyd-Dunyaa.
- Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 111-113
- Imechapishwa: 23/12/2024

Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 111-113
Imechapishwa: 23/12/2024
https://firqatunnajia.com/24-nyamazia-magomvi-ya-maswahabah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)