Swali: Nini hukumu ya adhaana inayotolewa na mwenye kutenda dhambi nzito?

Jibu: Maoni yaliyotagaa kati ya wanazuoni ni kwamba haisihi. Ni lazima muadhini awe mtu mwadilifu, ijapo kwa muonekano wa nje. Kwa sababu anatoa taarifa ya wakati wa swalah. Taarifa za watenda madhambi mazito hazikubaliwi. Ni lazima awe mwadilifu. Hata hivyo ikiwa kuna waadhini wengine katika mji wanaosikika na wanatosheleza, basi jambo hili ni jepesi zaidi. Hali ya kuwepo kwake ni sawa na kutokuwepo kwake. Lakini haifai kumpa jukumu la kutoa adhaana mahali ambapo watu wanamtegemea. Kwa hali yoyote haifai kabisa kumpa jukumu hili mtu ambaye ufisadi wake umebainika wazi. Haijuzu kupewa jukumu hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24787/حكم-اذان-الفاسق
  • Imechapishwa: 23/12/2024