Swali: Je, inajuzu kuzungumza na Khatwiyb siku ya ijumaa ikiwa amekosea katika Aayah au ninataka kumuuliza jambo?
Jibu: Hakuna ubaya. Hakuna tatizo kumuuliza Khatwiyb kuhusu baadhi ya masuala, kama walivyofanya Maswahabah kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa anakhutubu siku ya ijumaa, akamjia mtu akasema:
”Ee Mtume wa Allaah! Mali zimeangamia na njia zimekatika. Hivyo basi muombe Allaah atuletee mvua.”’
Basi akaomba msaada kwa ajili ya waislamu na akamuomba Allaah awanusuru waja (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo Allaah akawaletea mvua.
Wakati mwingine akamjia mara nyingine mtu naye anakhutubu kwa watu akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Amekuja mgeni anauliza kuhusu dini yake hajui dini yake ni ipi?” Basi akashuka na akamfundisha, kisha akarudi katika Khatwiyb yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kwa hiyo ninachotaka kusema ni kwamba hakuna ubaya kumuuliza kuhusu jambo wakati anakhutubu. Aidha hakuna kizuizi kumjibu ikiwa amekosea katika Aayah ambapo ukamkumbusha juu ya hilo. Hilo halina ubaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3467/حكم-التحدث-مع-خطيب-الجمعة-اثناء-الخطبة-لحاجة
- Imechapishwa: 03/09/2026
Swali: Je, inajuzu kuzungumza na Khatwiyb siku ya ijumaa ikiwa amekosea katika Aayah au ninataka kumuuliza jambo?
Jibu: Hakuna ubaya. Hakuna tatizo kumuuliza Khatwiyb kuhusu baadhi ya masuala, kama walivyofanya Maswahabah kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa anakhutubu siku ya ijumaa, akamjia mtu akasema:
”Ee Mtume wa Allaah! Mali zimeangamia na njia zimekatika. Hivyo basi muombe Allaah atuletee mvua.”’
Basi akaomba msaada kwa ajili ya waislamu na akamuomba Allaah awanusuru waja (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo Allaah akawaletea mvua.
Wakati mwingine akamjia mara nyingine mtu naye anakhutubu kwa watu akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Amekuja mgeni anauliza kuhusu dini yake hajui dini yake ni ipi?” Basi akashuka na akamfundisha, kisha akarudi katika Khatwiyb yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kwa hiyo ninachotaka kusema ni kwamba hakuna ubaya kumuuliza kuhusu jambo wakati anakhutubu. Aidha hakuna kizuizi kumjibu ikiwa amekosea katika Aayah ambapo ukamkumbusha juu ya hilo. Hilo halina ubaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3467/حكم-التحدث-مع-خطيب-الجمعة-اثناء-الخطبة-لحاجة
Imechapishwa: 03/09/2026
https://firqatunnajia.com/kuongea-na-khatwiyb-wakati-wa-khutbah-kwa-sababu-ya-haja/