Swali: Mimi ninapokea mshahara wa kiasi cha 6,500 SAR, lakini kazi ninayofanya ni kidogo sana na nafsi yangu haijatulia kwa sababu kipato cha kila siku ni takriban 200 SAR na huenda nisifanye kazi yoyote siku hiyo. Je, niache kazi au nifanye nini? Na ninahisi kuwa du´aa zangu hazijibiwi kwa sababu ya kula mshahara huu bila ya kazi iliyo wazi?
Jibu: Ikiwa unatekeleza kile ulichoajiriwa kwa ajili yake na Allaah amekurahisishia kazi ambayo haina uzito, basi mshukuru Mola wako kwa hilo. Ikiwa Allaah amekurahisishia kazi nyepesi na ameridhia mwenye kukuajiri na mwenye kuajiriwa kwa ujira huu, kisha unasema kuwa hutaki urahisi na badala yake unataka ugumu? Ikiwa amekutumia kwa ujira wa kila siku 200 au 1,000 kwa kazi nyepesi juu yako, basi hii ni katika fadhilah za Allaah juu yako. Hakuna ubaya ndani yake. Ikiwa hakuna khiyana wala kitu chochote na umetimiza wajibu.
Ikiwa amekuletea uwe mlinzi wa mlango na anakupa kila siku 200 na wewe ni mlinzi uko huru haikudhuru katika hili, basi akuna ubaya juu yako. Ikiwa amekuletea uwe dereva na akakupa 1,000 au 2,000 na wewe huendeshi isipokuwa mara moja kwa siku au baadhi ya siku huendeshi, basi mshukuru Allaah. Kusudi ni kwamba hakuna ubaya, ewe mwanangu, ikiwa umetimiza wajibu uliowekewa sharti. Huna kosa hata kama ujira ni mkubwa. Hii ni katika fadhilah za Allaah juu yako.
Lakini kimebaki kitu kilicho wazi nacho ni yule anayefanya kazi ya ziada juu ya kazi aliyoajiriwa kwa ajili yake. Asili yake ni uhalali na kuruhusu. Lakini huenda kukawa na mambo yanayozuia kufanya kazi, ikiwa kazi yake ya ziada inaathiri kazi yake rasmi, hili linaangaliwa. Ni lazima kuangaliwa. Huenda dola imeweka katika hili jambo fulani au imeainisha katika hili jambo fulani.
Kwa kumalizia ni kwamba ikiwa kazi yake ya ziada haiathiri kazi yake ambayo aliletwa kwa ajili yake, hatujui ndani yake kizuizi cha Kishari´ah. Ama ikiwa kazi yake ya ziada inaathiri kazi yake aliyokuja kwa ajili yake, kwa maana anafanya kwa mfano kazi nyingi zinazomchosha. Akija kazi ambayo aliletwa kwa ajili yake anasema mimi nimechoka sina nguvu, basi hili halifai. Ni lazima kazi yake ya ziada isiathiri kazi yake aliyokuja kwa ajili yake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3460/vحكم-اخذ-اجر-كبير-على-عمل-خفيف
- Imechapishwa: 03/09/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3460/vحكم-اخذ-اجر-كبير-على-عمل-خفيف
Imechapishwa: 03/09/2026
https://firqatunnajia.com/kupokea-pesa-kubwa-kwa-pesa-nyepesi/