20 – Muhammad bin Yahyaa bin ´Abdillaah ametukhabarisha: Ya´quub bin Ibraahiym ametukhabarisha: Baba yangu ametukhabarisha, kutoka kwa Swaalih, kutoka kwa Ibn Shihaab: Abu Umaamah bin Sahl amenihadithia ambaye amehadithia kuwa amemsikia Abu Sa´iyd al-Khudriy akisimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Wakati nilipokuwa nimelala niliota watu wakiwa wamevaa makanzu marefu. Kuna zilizokuwa zinafika kifuani, zingine zinafika chini ya hapo.” ´Umar bin al-Khattwaab akadhihirishwa kwangu – alikuwa amevaa kanzu refu ilikuwa ikiburuta.” Wakasema: ”Unaifasirije hiyo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Dini.”[1]
21 – Nuuh bin Habiyb ametukhabarisha: ´Abdur-Razzaaq ametuhadithia: Ma´mar ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Wakati nilipokuwa nimelala niliota kuwa naletewa kikombe nikanywa humo mpaka nikaona kinywaji kinatoka nje. Kisha nikampa nilichobaki ´Umar.” Wakasema: ”Unaifasirije hiyo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Dini.”[2]
22 – ´Amr bin ´Uthmaan amenikhabarisha: Baqiyyah ametuhadithia: az-Zubaydiy amenihadithia: az-Zuhriy amenikhabarisha, kutoka kwa Hamzah bin ´Abdillaah bin ´Umar, kutoka kwa Ibn ´Umar, ambaye amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Wakati nilipokuwa nimelala niliota napewa kikombe cha maziwa. Nikanywa humo mpaka nikaona kinywaji kinatiririka kwenye kucha zangu. Kisha nikampa nilichobaki ´Umar.” Wakasema: ”Unaifasirije hiyo?” Akasema: ”Dini.”
[1] al-Bukhaariy (23) na Muslim (2390).
[2] al-Bukhaariy (3681) na Muslim (2391).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 40-41
- Imechapishwa: 03/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 40-41
Imechapishwa: 03/09/2026
https://firqatunnajia.com/04-dini-na-elimu-ya-umar/