14 – Muhammad bin Aadam amenikhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametuhadithia, kutoka kwa ´Umar bin Sa´iyd, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah: Nimemsikia Ibn ´Abbaas akisema:
”´Umar aliwekwa kwenye kitanda chake cha jeneza. Watu wakasongamana, wakimuombea du´aa, kumsifu na kumswalia kabla hajanyanyuliwa kuondoshwa pale. Nilikuwa miongoni mwao. Tahamaki bwana mmoja akanishika begani kwa nyuma yangu. Nikageuka na kuona kuwa ni ´Aliy. Akimuombea rehema ´Umar na kusema: ”Hujamwacha yeyote ambaye matendo yake yananipendeza zaidi kukutana na Allaah nikiwa nayo kama matendo yako. Naapa kwa Allaah! Naonelea kuwa Allaah akujaalie kuwa pamoja na marafiki zako, kwa sababu mara nyingi nilikuwa nikimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Mimi, Abu Bakr tuliondoka…”, ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tuliingia… ” na ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tulitoka… ” Kwa hivyo naonelea kuwa Allaah akujaalie kuwa pamoja na marafiki zako.”[1]
15 – ´Umar bin ´Uthmaan ametukhabarisha: Muhammad bin Harb ametuhadithia, kutoka kwa az-Zubaydiy, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Sa´iyd aliyehadithia kwamba Abu Hurayrah amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Wakati nilipokuwa nimelala niliota nimesimama karibu na kisima kilichokuwa na ndoo. Nikachota kutoka humo kile kiasi alichotaka Allaah. Kisha Ibn Abiy Quhaafah akachota ndoo moja au mbili. Uvutaji wake ulikuwa na unyonge. Allaah amsamehe. Kisha ndoo ikawa kubwa na ´Umar bin al-Khattwaab akaichukua. Sikumuona bwana yeyote aliyechota kama alivochota ´Umar bin al-Khattwaab – hatimaye watu wakajenga shimo la maji.”[2]
16 – ´Ubaydullaah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Yahyaa bin Hammaad ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin al-Mukhtaar ametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid al-Hadhdhwaa’, kutoka kwa Abu ´Uthmaan: ´Amr bin al-´Aasw amenihadithia:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniteua kuwa kiongozi juu ya jeshi lililotumwa kwenda Dhaat-us-Salaasil. Nikamwenda na kusema: ”Ee Mtume wa Allaah, ni mtu gani anayependeza zaidi kwako?” Akasema: ”´Aaishah.” Nikasema: ”Katika wanaume?” Akasema: ”Baba yake.” Nikasema: ”Kisha nani?” Akawataja baadhi ya wanaume.”
Baadhi ya herufi za Abu ´Uthmaan hazikusihi.
17 – Zakariyyaa bin Yahyaa ametukhabarisha: Ishaaq ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha: Abul-´Umays ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah, kutoka kwa ´Aaishah, aliyehadithia:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliaga dunia bila ya kumteua yeyote kuwa khaliyfah baada yake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Kama ningelimwacha yeyote kuwa khaliyfah baada yangu, basi ningelimwacha khaliyfah Abu Bakr na ´Umar.”[3]
18 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: al-Layth ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa Sa´d bin Ibraahiym, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa ´Aaishah: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Katika ummah kulikuwa na watu wenye kuhamasisha. Kama katika ummah wangu kungelikuwa na mtu yeyote mhamasishaji, basi angelikuwa na ´Umar bin al-Khattwaab.”[4]
19 – Muhammad bin Raafiy´ na al-Hasan bin Muhammad wametukhabarisha: Sulaymaan bin Daawuud ametuhadithia: Ibraahiym – Ibn Sa´d – ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Nyumati zilizotangulia kabla yenu zilikuwa na watu wenye kuhamasisha. Kama ummah wangu huu angelikuwepo yeyote katika wao, basi angelikuwa ni ´Umar bin al-Khattwaab.”
[1] Ahmad (1/112), al-Bukhaariy (3677) na Muslim (2389).
[2] al-Bukhaariy (7019) na Muslim (2393).
[3] Muslim (2385).
[4] Muslim (2398).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 38-40
- Imechapishwa: 03/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 38-40
Imechapishwa: 03/09/2026
https://firqatunnajia.com/03-mimi-abu-bakr-na-umar/