Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: Abu Daawuud al-Hifriy ´Umar bin Sa´d ametukhabarisha: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-A´raj, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Wakati bwana mmoja alipokuwa anamchunga ng´ombe na akataka kumpanda, ambapo akasema: ”Sisi hatukuumbwa kwa lengo hili; hakika sisi tumeumbwa kwa ajili ya kilimo.” Watu waliokuwa pembezoni mwake wakasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!  Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.” Hawakuwepo pale. Akasema: ”Wakati bwana mmoja alipokuwa kati ya kondoo wake tahamaki akaja mbwa mwitu na kumchukua kondoo mmoja. Bwana yule akamfata kwa ajili ya kumchukua, ambapo mbwa mwitu yule akasema:  ”Nini utachofanya siku ya Wanyama wakali ambayo hakutokuwepo mchungaji mwingine zaidi yangu?” Watu waliokuwa pembezoni mwake wakasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!  Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.” Hawakuwepo pale.”[1]

11 – Haaruun bin Muhammad bin Bakkaar bin Bilaal ametukhabarisha, kutoka kwa Muhammad bin ´Iysaa (yaani Ibn-ul-Qaasim bin Samiy´): ´Ubaydullaah bin ´Umar ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwageukia watu akasema: ”Wakati bwana mmoja alipokuwa anamchunga ng´ombe na akataka kumpanda, ambapo akamgeukia na kusema: ”Sisi hatukuumbwa kwa lengo hili; hakika sisi tumeumbwa kwa ajili ya kilimo.” Watu waliokuwa pembezoni mwake wakasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu! Ng´ombe amezungumza!” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.” Hawakuwepo pale. Akasema bwana mmoja: ”Wakati bwana mmoja alipokuwa kati ya kondoo wake tahamaki akaja mbwa mwitu na kumchukua kondoo mmoja. Nikamfata na kumchukua, ambapo akanambia:  ”Nini kitachomtokea siku ya Wanyama wakali ambayo hakutokuwepo mchungaji mwingine zaidi yangu?” Wakasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu! Mbwa mwitu amezugnumza!” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.” Hawakuwepo pale.”

12 – ar-Rabiy´ bin Sulaymaan ametukhabarisha: Shu´ayb bin al-Layth ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesema:

”Pindi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomaliza kuswali, akawageukia Maswahabah wake na kusema: ”Wakati bwana mmoja alipokuwa anamchunga ng´ombe na akataka kumpanda, ambapo akasema: ”Sisi hatukuumbwa kwa lengo hili; hakika sisi tumeumbwa kwa ajili ya kilimo.” Watu waliokuwa pembezoni mwake wakasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!  Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.” Hawakuwepo pale. Akasema: ”Wakati bwana mmoja alipokuwa kati ya kondoo wake tahamaki akaja mbwa mwitu na kumchukua kondoo mmoja kutoka katika kondoo wake, ambapo mchungaji yule akamfata. Wakati alipomfikia, akamwachilia kutoka kwenye mdomo wake, akamgeukia na kusema: ”Ni nani atakuwa naye siku ya Wanyama wakali ambayo hakutokuwepo mchungaji mwingine zaidi yangu?” Watu waliokuwa pembezoni mwake wakasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!  Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.” Hawakuwepo pale.”

13 – Sulaymaan bin Daawuud ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Wahb: Yuunus amenikhabarisha, kutoka kwa Ibn Shihaab: Sa´iyd bin al-Musayyab na Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan wametukhabarisha kuwa wamemsikia Abu Hurayrah akisema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Wakati bwana mmoja alipokuwa akimchunga ng´ombe akampanda, ambapo ng´ombe yule akamgeukia na kusema: ”Mimi sikuumbwa kwa lengo hili; hakika sisi tumeumbwa kwa ajili ya kilimo.” Watu wakashangazwa na kusema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!  Ng´ombe anazungumza!” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.” Abu Hurayrah amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Wakati mchungaji mmoja alipokuwa kati ya kondoo wake, mbwa mwitu akamrukia kondoo mmoja na kumchukua, mchungaji yule akamfata kwa ajili ya kumwokoa. Mbwa yule akamgeukia na kusema: ”Ni nani atakuwa naye siku ya Wanyama wakali ambayo hakutokuwepo mchungaji mwingine zaidi yangu?” Watu wakasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu!” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi, Abu Bakr na ´Umar tumeyaamini.”

[1] al-Bukhaariy (3663) na Muslim (2388).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 03/09/2026