Swali: Vipi ikiwa maiti aliye katika Ihraam atafunikwa kwa sanda ya kawaida?

Jibu: Watafunika kichwa chake siyo?

Swali: Ndiyo, walifunika kichwa chake kwa sanda ya kawaida na si kwa Ihraam?

Jibu: Si jambo la mbali. Ikiwa hayo yamefanyika si muda mrefu sana, basi hapana vibaya kufukuliwa na kichwa chake kiondolewe kufuniko. Lakini ikiwa muda mrefu umeshapita, hakuna haja ya kufanya hivyo. Hata hivyo ikiwa bado ni mapema na mwili haujabadilika, basi hakuna kizuizi cha kuondoa sanda kichwani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24962/حكم-تكفين-الميت-المحرم-في-الثياب-المعتادة
  • Imechapishwa: 13/01/2025