Swali: Vipi tutaonisha kati ya utumiaji wa ´Aaishah wa manukato ilhali wanawake wamekatazwa kutumia manukato?

Jibu: Manukato yasiyodhuru ni yale ambayo harufu yake haihisiki waziwazi kwa watu. Wanawake wanaweza kutumia manukato wanapokuwa peke yao na hawako mbele ya wanaume. Manukato yanayokatazwa ni yale yanayojulikana kwa harufu yake kwenye masoko, kati ya watu au mbele ya wanaume.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24960/ما-الذي-يسمح-به-من-الطيب-للنساء
  • Imechapishwa: 13/01/2025