Swali: Je, anaweza kutoka kwenye Ihraam mtu aliyekwama na hakuweza kupata mnyama wa kuchinja?

Jibu: Anapaswa kufunga siku kumi kisha anyoe nywele au apunguze na hapo anaweza kutoka kwenye Ihraam. Ikiwa hana mnyama wa kuchinja, atafunga siku kumi kisha anyoe nywele au apunguze nywele na hapo anaweza kutoka kwenye Ihraam.

Swali: Je, kufunga kunapaswa kufanyika kabla ya kutoka kwenye Ihraam?

Jibu: Ndio, badala ya kuchinja mnyama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24963/حكم-من-احصر-ولم-يجد-الهدي
  • Imechapishwa: 13/01/2025