Swali: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا

“Ikiwa wawili nyinyi mtatubia kwa Allaah, basi hakika nyoyo zenu zimeelemea.”[1]

Kisha baada ya hapo akasema:

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا

“Akikutalikini, basi wajibu kwa Mola Wake kumbadilishia wake bora kuliko nyinyi; waislamu, waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wafanya ‘ibaadah, wafungao na wanaohajiri, wajane na mabikra.”[2]

Je, hapa kuna dalili ya kufaa kumtishia talaka mwanamke?

Jibu: Ndio. Mume ni mwenye kumiliki talaka. Hapana neno akimtishia. Pengine kufanya hivo kukamnyoosha.

[1] 66:04

[2] 66:05

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22366/ما-حكم-التهديد-بالطلاق
  • Imechapishwa: 24/02/2023