Bora ni kumrekebisha mke mbali na kumpiga

Swali: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَاضْرِبُوهُنَّ

“… na wapigeni.”

Jibu: Ni kwa njia ya ruhusa:

وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ

“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni.”[1]

Swali: Ni kamilifu zaidi kutowapiga?

Jibu: Ndio. Ikiwa kumtengeza pasi na kumpiga ndio bora zaidi.

Swali: Kusamehe wakati wa mtu kutokuwa na uwezo?

Jibu: Huko hakuitwi kusamehe. Ni kushindwa. Kusamehe kunakuwa pale mtu anapokuwa na uwezo. Lakini asipokuwa na uwezo kunaitwa kushindwa.

[1] 04:34

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22376/ما-معنى-قوله-تعالى-واضربوهن
  • Imechapishwa: 24/02/2023