Kumtembelea mgonjwa aliyelala koma/ICU

Swali: Anatembelewa mgonjwa ambaye amelala koma/ICU na hamjui anayemtembelea?

Jibu: Hakuna faida. Kwa sababu malengo ya matembezi ni kumuuliza hali yake na kumliwaza. Huyu hakuna faida labda kumuombea du´aa. Ukimtembelea ilihali yuko na utambuzi analiwazika nawe na anaona kuwa unamjali. Lakini akiwa hana hisia basi hakuna faida ya matembezi. Hakuna kilichobakia isipokuwa kumuombea du´aa ya uzima na ponyo.

Swali: Amuombee wakati wa kuwa mbali naye?

Jibu: Hapana vibaya akimuombea katika uwepo mbali naye.

Swali: Vipi kumsomea Qur-aan?

Jibu: Akimsomea Qur-aan Allaah amlipe kheri. Akimsomea Qur-aan ni mema mengine mbali na matembezi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21984/هل-يزار-المريض-الغاىب-عن-الوعي
  • Imechapishwa: 08/10/2022