Hapa ndipo atatoka Ya´juuj na Ma´juuj

Swali: Kutoka kwa Ya´juuj na Ma´juuj ni katika alama za Qiyaamah?

Jibu: Ndio. Ni miongoni mwa zile alama zake kubwa. Lakini ni miongoni mwa zile alama kubwa kumi za mwanzo za Qiyaamah; baada ya al-Mahdiy, baada ya ad-Dajjaal, baada ya kushuka kwa ´Iysaa ndipo atatoka Ya´juuj na Ma´juuj. Ni alama ya nne. Kipindi cha ´Iysaa mwana wa Maryam ndipo atatoka Ya´juuj na Ma´juuj:

وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ

“… ilihali kutoka kila mwinuko watateremka.”[1]

Watatoka upande wa mashariki.

[1] 21:96

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21980/هل-خروج-ياجوج-وياجوج-من-اشراط-الساعة
  • Imechapishwa: 08/10/2022