Swali: Wako wanaofikiri kuwa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni siku ya ijumaa peke yake.

Jibu: Hapana, ni kila wakati. Ni yenye kuenea. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.”[1]

Ni yenye kuenea katika nyakati zote; usiku na mchana, katika hali ya safari na hali ya ukazi, umeketi, umeegemea au unatembea. Ni kama mfano wa kumtaja Allaah. Ni aina fulani ya kumtaja Allaah.

Swali: Lakini inapendeza kumswalia kwa wingi siku ya ijumaa?

Jibu: Ataongeza zaidi. Kama mfano wa alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Niswalieni kwa wingi siku ya ijumaa.”[2]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy” (08).

[2] Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy” (28).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23006/هل-فضل-الصلاة-والتسليم-يختص-بالجمعة
  • Imechapishwa: 07/10/2023