Swali: Imamu akiswali ´Aswr na akasimama katika Rak´ah ya tano. Je, maamuma amfuate?

Jibu: Hapana. Maamuma akijua kuwa imamu amezidisha, basi asimfuate. Akimfuata swalah yake inabatilika. Anatakiwa kuketi chini na ima atoe salamu kivyake au amsubiri imamu na kutoa salamu pamoja naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 01/09/2023