01. Ni vipi ukoo wa Mtume wetu upande wa baba?

Swali 1: Vipi ukoo wa Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) upande wa baba?

Jibu: Jina lake anaitwa Muhammad, mwana wa ´Abdullaah, mwana wa ´Abdul-Muttwalib, mwana wa Haashim, mwana wa ´Abdu Manaaf, mwana wa Quswayy, mwana wa Kilaab, mwana wa Murrah, mwana wa Ka´b, mwana wa Lu-ayy, mwana wa Ghaalib, mwana wa Fihr, mwana wa Maalik, mwana wa an-Nadhwr, mwana wa Kinaanah, mwana wa Khuzaymah, mwana wa Madrakah, mwana wa Ilyaas, mwana wa Madhwarr, mwana wa Nazaar, mwana wa Ma´ad, mwana wa ´Adnaan anayetokana na kizazi cha Ismaa´iyl, mwana wa Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 91
  • Imechapishwa: 01/09/2023